Wakaaji wa Uvira wanaitajika ku pokea vizuri watumishi wa mtaa wa Afya ya uvira watakaopita nyumba kwa nyumba Katika Hali ya kufanya utafiti kuusu ugonjwa wa kipindupindu.
Published on Sunday 27 March 2022 - 11:00
Mtaa wa Afya ya Uvira, kwa kushirikiana na Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Kipindupindu na Magonjwa ya Kuhara, Taasisi ya Usafi na Tiba ya Tropiki ya London ya Uingereza na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani, inaandaa utafiti Katika makata za jiji la uvira kwaku jaribu kuelewa vyema jinsi kipindupindu kinavyoenea katika Uvira, jinsi watu hutafuta matibabu ya kuhara, na jinsi chanjo ya kipindupindu na hatua nyinginezo zinaweza kusaidia kukomesha kuenea kwake.
Tafiti hizi zitafanyika kuanzia mwisho wa Machi na
mwezi mzima wa Aprili 2022. Wakati wa tafiti hizi, timu
kutoka eneo la afya la Uvira zitatembelea baadhi ya manyumba
zilizochaguliwa ili kuwahoji wanainchi wote wenye umri
wa mwaka 1 au zaidi kuhusu magonjwa ya kuhara, ikiwa ni
pamoja na :kipindupindu, upatikanaji wa maji safi ya kunywa
na vifaa vya kutosha vya usafi, matumizi ya huduma za afya
kwa magonjwa ya kuhara.
Tafiti hizi pia zitaiwezesha Wizara
ya Afya kuelewa iwapo wananchi wamepata chanjo ya
kipindupindu na iwapo chanjo hii imepunguza hatari ya kupata
kipindupindu katika jiji letu. Kushiriki katika tafiti hizi ni kwa
hiari kabisa. Hakuna chanjo itakayotolewa kwa idadi ya watu
wakati wa tafiti hizi.
Tunaomba idadi ya watu ikaribishe timu
za wachunguzi ili kwa pamoja tuelewe jinsi ya kupambana
vyema na kipindupindu katika jamii yetu.
Mtaa wa afya wa Uvira.
Les Articles Recents
Publié le 04/02/2026 - 09:29
Publié le 03/02/2026 - 18:50
Uvira : MICHE-asbl forme des femmes leaders communautaires sur la paix et la cohésion sociale.
Publié le 03/02/2026 - 17:52
Publié le 29/01/2026 - 21:54
Publié le 29/01/2026 - 21:35
